UTANGULIZI
Migomba huzaa zao ambalo huitwa ndizi, ndizi huliwa kwa kupikwa, kukaushwa, kuvundikwa au kwa kusangwa na kutengeneza unga wake.
HALI YA HEWA NA UDONGO
Migomba hustawi vizuri kwenye maeneo joto kati ya 25oC hadi 30oC na huitaji mvua 1000mm kwa mwaka, pia uitaji udongo ulio na rutuba na unyevu wa kutosha. katika hali tajwa hapo juu mgomba unauwezo wa kuzaa matunda kati ya miezi 8 hadi 12 baada ya kuhamishia shambani(transprating). katika hali ambayo sio nzuri migomba inaweza kuchukua mda kidogo kuzaa hadi miezi 18. kwa hapa Tanzania migomba hustawi vizuri katika mikoa ya moshi, kagera na mbeya
AINA
kuna aina mbili za ndizi
- aina ya dessert
- aina ya plantain
plantain- hii ni aina ambayo ni nzuri zaidi kwa kupika mfano mzuzu na mkono wa tembo
KUPANDA
Migomba mara nyingi haiitaji mbegu kupanda, hupandwa kwa kutumia sucker, hivi ni ni vimigomba vidogo ambavyo vinakua pembeni, inatakiwa kuchukua watoto wenye urefu wa 1/2 na ikiwa na upana 15cm hadi 25cm na zingatia kuchagua mimea yenye afya.
migomba hupandwa mwanzoni mwa masika, chagua sucker katika aina unayo itaji.
chimba mashimo yenye urefu na upana wa 60cm, mashimo yanatakiwa kua na umbali ufatao
- aina fupi 3m x 3m
- aina ya kati 3m x 4m
- aina ndefu 4m x 4m
MBOLEA
Weka vijiko vikubwa 5 hadi 7 ya mbolea ya CAN kwa kila mmea kwa kila mwaka, anza kuweka mbolea kuanzia mwaka wa pili kutoka kupanda, zungushia mboelea kwenye mmea kwa umbali wa 4cm kutoka kwenye mmea.
KUPALILIA, KUNGOLEA NA KUFUNIKIA
Shamba la migomba hutakiwa kua safi na kutokua na magugu mda wote, unapo palilia zingatia kutoathiri mizizi ya mmea ambayo hukua umbali wa 15cm kutoka juu ya ardhi.
ili kuongeza ukubwa wa ndizi na ubora punguza mashina na kubakiza shina moja katika kila mgomba.
mashina ambayo hukwatwa wakati wa kupuynguzia yanaweza kutumika kufunikia mmea, kufunikia husaidia kupunguza mmommonyoko wa udongo, kuhifadhi unyevu na pia husaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa magugu.
KUWEKEA MTI WA KUZUIA
Pale mgomba unapobeba mkungu mzito na mkubwa na muhimu kuwekea mti wa kuegeshea ili kuusapport mgomba.
MAGONJWA NA WADUDU
wadudu wakuu katika migomba ni
- nematode
- weevel wa migomba
ugonjwa wa panama
unaweza kuwasiliana na mtaalamu moja kwa moja ili kufahamu zaidi jinsi ya kukabiliana na wadudu na magonjwa kwa kubofya HAPA
KUVUNA
kata shina la mgomba pale ndizi zinapo komaa na kabla hazijawa za njano, pia baada ya kuvuna kata shina kubwa na yape nafasi mashina yanayo anza kuota.
nitumaini langu umejifunza usisite kutembelea UKURASA WETU kila siku kwa kujifunza mengi zaidi
USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI BONYEZA LINK HII KUDOWNLOAD ==> http://ift.tt/2tqvrGF
No comments:
Post a Comment