KUTUMIA MIKOO KUATAMISHIA MAYAI.
Karibu Ndugu katika somo hili na hii ni;
Sehemu 2.
Sehemu ya kwanza tuliona kuwawekea mikoo mayai hata kama hawajaanza kutaga kwa kuwafunika na tenga ,ili kesho yake uone ni yupi atakaye toa mrejesho mzuri.
Katika sehemu ya pili tunaongelea kutumia njia ya kuwa subirisha:
Ufugaji kuku hasa watu walio vijijini wana changamoto ya upatikanaji wa machine za kutotolesha, na hivyo kuzalisha kuku wengi kwa muda mchache kwao huwa ni changamoto.
Hii hutokana na mawazo yao au mifumo wanayo tumia kulea Vifaranga, mfumo wa kuacha Vifaranga vilelewe na mama yao wengi huupenda,Ila ni moja ya mfumo unaochelewesha kuku kuzaliana.
Ndugu Mfugaji hata kama hauna machine ya kutotesha tambua bado unao uwezo wa kukuza mradi wako.
Pia tambua na ujue siku zote kuwa Ufugaji unahitaji ubunifu zaidi ya ubunifu uwe na lengo na nia ya kuthubutu.
Kuna vitu unaweza ona vikifanywa na mfugaji kama kutengeneza mchwa , funza, fodder nk ; ukamuona ni kama anajisumbua ila utakapo jua umuhimu wake tayari utakuwa umechelewa na huyo mfugaji kwako atakuwa ni mfano wa kuuiga.
Katika kutumia njia hizi ni lazima uwe na lengo , nia ya kuthubutu ili ufanikishe; nani muhimu kutanza kumbukumbu idadi ya kuku, utagaji na matumizi ya matunzo.
Twende katika njia hiii ya kusubirisha , kwanza kabisa hii njia itakufanya upate Vifaranga wengi kwa pamoja na jinsi ya kuvitunza kwenye chakula na chanjo inatakuwa ni rahisi.
Kuna watu hupata changamoto katika kuku kutotoa kwa kutofautiana siku , unaweza kuta Vifaranga hawa wana siku 3 ,wale wana wiki , wengine wana siku 14. Kwahiyo hapo utapata changamoto kubwa kwenye kuwapa chanjo kama ulikuwa pamoja nami kuanzia sehemu ya kwanza mpaka hii ya pili natumaini utakuwa umesha pata mwanga jinsi ya kudhibiti changamoto hii.
SEHEMU YA PILI
_ Kuwa makini kuchunguza ili ujue kuku atakae anza kutaga
_ Andaa trey na sehemu safi isiyo na joto kwaajili ya kuhifadhi mayai
_Kuku yeyote atakaye anza kutaga ili sehemu anapo taga weka yai vinza kisha mayai anayo taga kila siku uwe unayatoa na kuhifadhi kwenye trey
_Wakati wakushika mayai hakikisha mikono unapaka majivu au shika na kitambaa kisafi, kikavu kishicho na harufu ya mafuta
_ Kwenye kuhifadhi mayai hakikisha ile sehemu iliyo chongoka ndio inayo elekea chini
_Katika kuhifadhi mayai weka kumbukumbu ili ujue mayai haya ya kuku fulani na alianza kutaga siku fulani, kurahisisha hili kila mayai ya kuku fulani yaweke pekeyake ili iwe rahisi kukumbuka
_Kila kuku atakaye anza kutaga utafanya hivyo kutoa mayai
_Mpaka watakapo fika idadi ya kuku unao taka uwasubirishe ili watotoe pamoja
_Kuku yoyote atakaye anza kuatamia utaacha aatamie lile yai viza kwa muda ili awasubiri wenzake
_ Weka kumbukumbu siku walizo achana kuku wako kwenye kutaga kutoka wa kwanza hadi wa mwisho
_ Utakapo ona wote wameanze kuatamia , andaa viota vizuri kulingana na idadi ya kuku wako
_ Kwenye kuwawekea mayai , hapa ndio sehemu muhimu zaidi kuwa makini na kumbukumbu , yule kuku alie tumia muda mwingi kuwasubiri wenzake mayai yake unaweza ukayala tu .kwasababu yatakuwa yamekaa muda mrefu na hivyo yanaweza yasitotolewe. Hivyo ni vizuri huyo kuku umuekee mayai mengine kutoka kwa wenzake.
_Kuku utawawekea mayai kulingana na umbo mayai 8,10,12 nk
_ Muda mzuri ni usiku kuku wote utawawekea mayai na wataanza kuatamia kwa pamoja
Siku ya kutotoa unaweza wawekea mayai mengine, hapo kazi ya kulea Vifaranga ni ya kwako
ZINGATIA: Maji na chakula viwepo karibu na viota vya kuku
Hakikisha kuku hawana wadudu wasumbufu kama utitiri,viroboto nk watakao wakosesha amani.
Nakutakia Ufugaji mwema
Mwisho wa somo hili ni mwanzo wa somo lingine
Whatsapp 0655610894
Gusa Hapa Kupakua App Ya Ufugaji Yakinifu Play Store
TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU
from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2AJ8fet
No comments:
Post a Comment