MADHARA YA KUTOKUPALILIA SHAMBA KWA WAKATI - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Tuesday, January 9, 2018

MADHARA YA KUTOKUPALILIA SHAMBA KWA WAKATI


Asante ndugu msomaji kwa kua nasi siku zote, na napenda kuanza kukupaelimu kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka huu.
na leo nitaelezea kuhusiana na hasara za kutokupalilia mapema na faidia za kupalilia shamba lako mapema.
Wakulima wengi sana wamekua wakilichukulia swala la kupalilia kama ni swala la hiali tu, lakini ukweli ni kwamba wewe kama mkulima na unalengo la kupata mazao mengi yenye ubora swala la kupalilia kwa wakati ni swala la muhimu sana hivyo ni muhimu kulizingatia.

   KUPALILIA-Kwa tafsiri rahisi kupalilia ni ilie hali ya kuondoa memea au majani ya saio itajika(magugu) shambani. kwa kitaalamu kitendo hiki kinaitwa (WEEDING).
Mkulia unaweza kuchagua njia sahihi ya kupalilia kulingana na uwezo, ukubwa wa shamba na aina ya mimea uliyo panda, kuna njia tofauti tofauti ya kupalilia kama zifuatazo
  • kwa kutumia jembe la mkono
  • kwa kutumia madawa(herbicides)
  • kwa kutumia jembe la ng'ombe
  • kwa kung'olea
usisite kuendelea kujifunza mengi zaidi kwa kujiunga moja kwa moja na blogi hii HAPA
  MAGUGU- magugu ni mmea wowote ule unao ota sehemu ambayo haiitajiki mfano kama shamba lako unapanda mpungu na ndani ya shamba ikawepo memea ya mahindi hivyo kwa wakati hua mahindi ni magugu na yanatakiwa kuondolewa shambani
pia kuna aina tofauti tofauti ya magugu kwa wakati mwingine nitakuletea somo la magugu na aina tofauti tofati ya magug, kwa somo letu la leo nitakuonesha kuhusiana na hasara za kutokupalilia kwa wakati muafaka.

MADHALA YANAYO YANAYO TOKANA NA UWEPO WA MAGUGU SHAMBANI
Kama nilivo elezea mwanza kua kuna hasara ya kutokupalilia kwa wakati, hivyo hapa nitaelezea hasara zinazo wezwa kulutwa na uwepo wa magugu shambani.
  • magonjwa
  • uwepo wa wadudu waharibifu
  • kugombea kwa virutubisho
  • kugombea kwa mwanga
  • kufa kwa mimea 
  • kupunguza ubora wa mazao 
  • na madhara makuu ni kukosa kwa mazao stahiki yaani kupata kidogo ukilinganisha na jinsi ulivo takiwa kupata.
NOTE; Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupalilia mapema na unaweza kupalilia mara mbili au zaidi kulingana na aina ya mmea au zao.
Unaweza kuwasiliana nasi kwa kupitia nambi hii
+255764148221
au unaweza kuwasiliana nasi kwa njia ya email kwa  kubofya HAPA


USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI BONYEZA LINK HII KUDOWNLOAD ==> http://ift.tt/2tqvrGF

No comments:

Post a Comment