MDUDU WA NYANYA KANITANGAZE.
Mdudu huyu anajulikana kama nondo wa nyanya na kitaalamu Tuta absoluta, aliyegungulika kuwepo nchini tangu 2014, lakini madhara yake yameanza kuonekana mwaka huu na ana athiri uzalishaji wa nyanya kwa kasi na kiasi kikubwa sana jambo lilopelekea wakulima kumbandika jina ‘kanitangaze’
Ni muhimu kwa wakulima kumtofautisha mdudu huyu na Yule mwenye mapindo, ambae kwa kawaida hushambulia nyanya na mazao mengine, wadudu wenye mapindo ni aina ya nzi –buu lake huzalisha kijumba chembamba, ambacho husukwa kwenye majani, lakini hakishambulii tunda kama ilivyo kwa Tuta absoluta .
TABIA ZA WADUDU HAWA.
Wadudu wakubwa wanafanya kazi usiku na mapema wakati wa asubui, Majira ya saa 1 hadi saa 5 asubuhi wanaweza kuonekana wakiruka kwenye sehemu ya juu ya majani.
Kwa kawaida huwa wanataga mayai usiku kwenye sehemu ya juu ya mimea, kwenye sehemu ya chini ya majani au shina changa au sehemu za maua, katika maisha yao, mdudu jike huweza kutaga hadi mayai 260.
Mayai yanapoanguliwa, mabuu hutumia masaa machache kujilisha juu ya mmea, baada ya hapo, wanaingia ndani ya mmea ambapo hukaa hadi wapevuke na kuwa wadudu wakubwa.
Baadhi ya mabuu walio kwenye pango walilopo na kuanzisha jingine, wakati mabuu walio kwenye mabadiliko huondoka kwenye pango walilopo na kuanzisha jingine, wakati mwingine ndani ya tunda, buu mmoja linaweza kuharibu tunda zima kwenye shada, wakati mabuu wanapozunguka mmea, wanafanya haraka sana kwa msaada wa nyuzi nyororo walizotengeneza.
UKUAJI.
Ukuaji wa buu hufanyika kwenye udongo na kwenye mimea yanyewe, mdudu anaepevuka kwenye mmea, hutengeneza kijumba chenye nyuzi laini ili kujikinda. Tuta absoluta ana kipindi cha miezi 12, katika maeneo yenye joto, mzunguko unaweza kukamilika chini ya mwezi mmoja.
Kutokana na muda wa mzunguko wa maisha kuwa mfupi, kuna hatua nyingi za mdudu huyu kuharibu mmea kwa kila kipindi kimoja cha maisha yake.
Wadudu hawa hawapendi baridi kali wala joto kali sana, Chini ya mwezi nyuzi joto 10 inazuia ukuaji Wa mdudu na ziadi ya nyuzi joto 30.
UHARIBU WAKE KWENYE SHAMBA
Wadudu hawa husababisha uharibifu enezi wa jani pamoja na tunda, ambao unaweza kusabaibishwa hasara ya asilimia 100 kwa mkulima, Mimea ya nyanya inashambuliwa kuanzia hatua za awali hupelekea hatua ya pili ya maambukizi ya kuvu na bacteria.
Buu linaweza kushambulia tunda mara tu linapotengenezwa, Huharibu pia vichipukizi ambavyo husababishwa ukuaji mbovu wa mimea.
UDHIBITI
Kwa kawaida utunzaji wote wa mazao hutegemea maamuzi madhibuti na utunzaji wa mazao, mdudu mharibifu anatakiwa asipate chakula kwenye mmea unaomhifadhi.
ILI KUMDHIBITI WADUDU HAWA ZINGATIA MAMBO MUHIMU YAFUATAYO.
- Usipande tena mazao, hifadhi mara tu baada ya uzalishaji wa mazao hifadhi ya mwanzo.
- Rudia kupanda mazao yasiyokuwa jamii ya mnavu.
- Unaweza kuacha eneo hilo kwa wiki 5 hali 6 bila kuwa na mimea hifadhi, Hali hiyo itasaidia kuondokaa kizazi cha wadudu hao katika eneo hilo.
- Ondoa magugu yote yenye majani mapana, weka mkazo kwenye kuondoa magugu jamii ya manavu.
- Ondoa nyanya zilizoharibiwa kutoka kwenye mmea na uzitekeketeze.
- Kuwa makini na utendaji wa majirani katika mashamba yao.
- Pangilia eneo lako vizuri kwa kuweka nafasi kutoka katika shamba la jirani.
SHUGHULI ZA BINADAMU.
Mdudu huyu anasambaa kwa haraka sana kutokana na shughuli za binadamu, ni muhimu kufanya juhudi ili kuzuia uenaji unaotokana na shughuli hizo.
Tuta absoluta wanaweza kutaga mayai kwenye miche iliyopo kwenye kitalu, Hivyo kabla ya kutoa miche kwenye ni lazima ichunguzwe kwa umakini, ili kuona kama kuna dalili za wadudu waharibifu.
Endapo wafanyakazi wamekuwa kwenye shamba lilizagaa wadudu, ni muhimu kuhakikisha kuwa hawabebi wadudu kwenye nguo zao kutoka eneo moja kwenda lingine.
Hakikisha kuwa hakuna tunda lililoathiriwa na mdudu linalopelekwa sokoni, Tunda liloharibika liteketezwe.
Vikapu na matenga yanayotumika kuvunia kwenye eneo safi ambalo halitaathiriwa.
VIATILIFU.
Kuna aina nyingi za viatilifu vinavyoweza kuua aina hii ya wadudu ‘ Tuta absoluta’ lakini kuna mambo mengi yanayowasaidia wasife kwa urahisi.
- Kanitangaze Tuta absoluta hujificha chini ya majani au tunda hali hii hufanya viatilifu vya mguso au kunyunyuziwa kushindwa kuleta mafanikio.
- Mdudu huyu hujenga uwezo kujenga uwezo wa kushindana na dawa zilizotumiwa kupita kipimo.
- Tumia acelamectin, katika matumizi ya kiatilifu hichi husichanganye na karate au dudu all, kwani wakulima wengi wamekuwa na tamaduni za kuchanganya viatilifu.
- Hivyo katika hutumiaji wa viatilifu hivi hakikisha unapuliza chini ya jani, pia puliza wakati wa jioni au asubuhi mapema wakati jua si kali, hakiksha unapulia kwa umakini.
- Wakati kupuliza hakikisha umevaa nguo maalumu kama viatu vya mpira (gumboot) glavu za mikononi, kofia, shati ya mikono mirefu hili kuepuka dawa hizi kuingia katika mwili/sehemu za mwili.
Ilikuweza kukabiliana na mdudu huyu, ni muhimu sana kutumia kiasi kidogo sana cha viatilifu kwa kuwa uwezo wa kujenga usugu kukabiliana na dawa hizo,au kutumia dawa za asili zinazoaminika kuwa na uwezo kujenga usugu kukabiliana na aina hiyo ya wadudu
Mchanganyiko Wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali na msaada Wa mtandao
from Kijana Endelevu Group http://ift.tt/2Ee3HOQ
USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YETU INAYOITWA KILIMO CHA KISASA SASA INAPATIKANA PLAY STORE BUREEE KABISA
No comments:
Post a Comment