SERIKALI KUIMARISHA MASOKO YA MAZAO-MAJALIWA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Saturday, February 3, 2018

SERIKALI KUIMARISHA MASOKO YA MAZAO-MAJALIWA



 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.
Aliyasema hayo jana (Februari 2, 2018) wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.
Alisema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko  ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.
“Kupitia Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao wanayolima.”
Alitoa mfano wa zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.
 Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Bw. Godfrey Malekano alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.
“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo.”
Alisema kufanikiwa kwa Soko la Bidhaa na Mfumo wa stakabadhi ghalani kunategemea sana msaada wa Serikali.  “Soko la Bidhaa la Ethiopia linalotajwa sana kwa mafanikio, limefikia malengo yake kutokana na mkono wa Serikali.”
Bw. Malekano alisema kutokana na umadhubuti wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wanamatumaini makubwa kwamba soko hilo  litatimiza malengo yake.


USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI BONYEZA LINK HII KUDOWNLOAD ==> http://ift.tt/2tqvrGF

No comments:

Post a Comment